HUDUMA ZA KITABIBU
Posted on: December 21st, 2024Idara ya Magonjwa ya ndani ndio yenye historia ndefu Zaidi tangu kipindi cha Ukoloni ambapo Mwanzilishi wa Hospitali alipata msukumo mkubwa uliotokana na vifo vingi mkoani Tanga vilivyoletwa na moja kati ya magonjwa yananyotibiwa na Idara hii. Kwa wakati wote tngu kipindi hicho, Idara imekua ikitoa huduma Mathubuti/stahiki kwa wagonjwa wa nje na waliolazwa zenye kuhusisha kinga, matibabu na huduma boreshi kwa magonjwa yasiyo na tiba.
Idara inapatikana katika Sakafu ‘A’ ya Jengo la Galanos ambapo ndipo zilipo wodi A1 na A2 zinazohudumia wagonjwa wanaume na wanawake waliolazwa, kitengo cha Afya ya akili kilichopo katika geti la Kuingilia Hospitalini, Gredi I iliyopo mkabala na jingo la zamani (Cliff) au Utawala na kitengo cha CTC kilichopo na ukumbi wa mikutano (Rhodassakis). Kitengo cha Wagonjwa wa ndani kinauwezo wa kulaza hadi wagonjwa 79 kwa mara moja ambapo ni jumuisho la vitanda 53 katika wodi A1 na A2, vitanda 15 vya gredi I na 11 vya wodi ya kitengo cha afya ya Akili.
Huduma kwa Wagonjwa wa Ndani
- Kupitia taratibu za uchunguzi wa kitabibu utambuzi wa magonjwa hufanyika na kuhakikisha matibabu sahihi hutolewa kwa kila mgonjwa.
- Mzunguko wa kuona wagonjwa Wodini: Hufanywa kila siku ikiwa ni pamoja na Mzunguko mkubwa ambao hufanyika kwa wiki mara moja.
- Mashauriano na Idara nyinginezo kwaajili ya utambuzujumla ki na matibabu ya magonjwa yenye muingiliano wa idara Zaidi ya moja.
Huduma kwa Wagonjwa wa Nje
Idara pia hutoa huduma za kawaida za magonjwa ya ndani na huduma mbalimbali za kibingwa kwa wagonjwa wanaohudhuria kliniki zetu. Kliniki hizi ni kama zifuatazo:
- Kliniki ya kawaida ya magonjwa ya ndani: Huduma ya Matibabu na kufuatilia maendeleo ya matibabu kwa wagonjwa walioruhusiwa na kwa magonjwa tofauti yasiyo ya dharura yenye kuhitaji kulazwa. Mfano: Presha ya kupanda, Baada ya Kiharusi, vidonda vya tumbo, Upungufu wa damu n.k. Hufanya kazi kwa siku mbili za wiki Jumanne na Ijumaa
- Kliniki ya Sukari: Huduma ya Matibabu na kufuatilia maendeleo ya matibabu kwa wagonjwa wa Kisukari. Hufanya kazi kwa siku zote za kazi katika wiki Jumatatu hadi Ijumaa, ambapo Jumatatu ni mahsusi kwaajijli ya watoto na vijana wenye Kisukari.
- CTC: mahususi kwaajili ya tiba na kujali wateja/wagonjwa na familia zilizoathirika na ugonjwa wa Ukimwi. Hufanya kazi kwa siku zote za kazi katika wiki Jumatatu hadi Jumamosi, ambapo Jumamosi ni mahsusi kwaajijli ya watoto na vijana.
Kliniki ya ngozi: Namna ya matunzo ya Afya ngozi na matibabu ya magonjwa mbalimbali ya ngozi hutolewa. Hufanya kazi kila jumatano.
Kliniki ya Afya ya Akili: Elimu, matibabu na ufuatiliaji wa magonjwa ya Akili hutolewa. Hutolewa kila siku ya wiki kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa
Huduma ya Mafunzo
Idara ya Magonjwa ya ndani kwa kushirikiana na Chuo cha Afya na Sayansi shirikishi pamoja na vyuo vinginevyo Mkoani Tanga inatoa mazingira mazuri kwaajili ya wanafunzi wa utabibu kujifunza kwa vitendo. Pia Hutoa mafunzo ya Utarajali kwa madaktari na wanafunzi kutoka nchi mbalimbali.
Huduma za kitabibu idarani hutolewa kwa ushirikiano baina ya Madaktari katika mafunzo ya utarajali (interns), matabibu (2) wenye mafunzo ya Saikolojia, AMO (3) madaktari (2) wakiongozwa na madaktari bingwa (2). Hadi wagonjwa 300 hutibiwa katiba wodi na kliniki zetu.