Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

Historia

  • Historia ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga 

Mnamo mwaka 1895 Dk. F. Plehn aligundua kuwa takribani 70% ya vifo kwa Tanga mjini vilisababishwa na malaria.  Aina kuu mbili za malaria kali (Cerebral malaria and black water fever) ndizo zilizokua sababu kuu za vifo vingi mjini Tanga. Kwa kipindi kile hakukuwepo Kituo cha afya (hospitali) kizuri hivyo wazo la kuwepo kwa hospitali lilizaliwa. Wazo lile liliwasilishwa kwa Dk. Alexander Berker, aliyekuwa Daktari  mkuu wa kwanza kwa Serikali ya Tanganyika.

Kabla ya ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Hoteli ya Liebels ambayo ilikuwepo mkabala na Hoteli ya Sea View ilikodiwa na kutumika kwa dharura kama hospitali.  Jengo lile lilitumika kwa kipindi kifupi tu kwa kuwa Dk. Alexander Berker alikua amekwisha kamilisha mipango kwaajili ya Hospitali ya Serikali  inayoendelea kutumika hadi leo.   Sehemu ya ardhi iliyokuwa Hoteli ya Liebels kwa sasa ni sehemu ya kituo cha kujazia mafuta.  Ujenzi wa Hospitali hii ya sasa ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ulianza mnamo mwaka 1896 na kukamilika miaka tisa baadaye.


Jengo la kwanza la Hospitali

Mnamo mwaka 1951 Ndg. Christas Galanos alichangia kiasi cha Euro 50,000 kwaajili ya ujenzi wa wodi kwaajili ya kina Mama na Watoto, na jiwe la msingi lilisimikwa na aliyekuwa Gavana, Sir Edward Twinning mwaka 1956.  Kazi ya ujenzi ilikamilika mnamo mwaka 1958.

Mnamo mwaka 1959, Rodoussakis alichangia fedha kwaajili ya ujenzi wa jengo la wodi yenye uwezo wa kukaa vitanda 52.  Jengo hili lilidhamiriwa kuwa kwaajili ya magonjwa ya kuambukiza (infectious diseases) hasa Kifua Kikuu.  Majengo mengine Zaidi yalijengwa mwaka 2007/2008 kwaajili ya wagonjwa wa nje, Chumba cha Upasuaji na matengenezo (OPD Complex, Operating Theatre, Maintenance Unit) kupitia msaada wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Mama na mtoto KfW. Kwa sasa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ndiyo kubwa kuliko Hospitali za Rufaa za Mikoa hapa Tanzania.