Mpango Binafsi wa kujifungua Salama
Posted on: October 18th, 2019ANDAA,ZUNGUMZA NA MWENZI WAKO,JAZA MPANGO
- Fahamu tarehe ya kujifungua.
- Fahamu na uhakikishe kituo cha kutolea huduma za afya au hospitali utakapojifungulia.
- Fanya mpango wa usafiri wa kukufikisha mapema kwenye kituo cha kutolea huduma za afya utakapojifungulia.
- Nani atakaye kusindikiza kwenye kituo cha kutolea huduma za afya mapema ili ujifungulie huko.
- Tayarisha mfuko utakapoweka nguo za mtoto na mahitaji yote wakati ukiwa katika kituo cha kutolea huduma za afya.
- Nani utakayemwachia nyumba utakapoenda kujifungua?
- Jadili na mwenza wako na mtoa huduma iwapo unataka kubadili mpango
ORODHA YA HUDUMA KWA MAMA MJAMZITO UENDAPO KLINIKI
- Vipimo vya kuzingatia kila uendapo kliniki
- Kipimo cha presha ya damu
- Kipimo cha kiwango cha damu
- Kipimo cha mkojo
- Mtoto anavyoendelea kukua tumboni
- Vipimo vinavyofanyika angalau mara moja wakati wa ujauzito
- Kipimo cha kundi la damu
- Kipimo cha magonjwa ya zinaa mfano Kaswende
- Kipimo cha Virusi Vya Ukimwi kwako na mwenza wako(kawaida mara mbili)
- Hakikisha unapata vitu hivi
- Chandarua chenye dawa( viatilifu)
- Chanjo za pepopunda
- Vidonge vya kuongeza damu(Tumia kila siku wakati wa ujauzito na endelea kutumia vidonge vya kuongeza damu mpaka miezi mitatu baada ya kujifungua)
- Dawa za minyoo(Tumia mara moja baada ya miezi mitatu ya ujauzito
- Vidonge vya SP kuanzia wiki ya 14 ya ujauzito na kila unapohudhuria kituo cha kutolea huduma za afya.
DALILI ZA HATARI KABLA YA KUJIFUNGUA/WAKATI WA KUJIFUNGUA/BAADA YA KUJIFUNGUA
- Uonapo dalili hizi nenda kituo cha kutolea huduma za afya mara moja!!!
- Kutoka damu ukeni
- Kuumwa sana na kichwa na kuona maluweluwe/kushindwa kuona
- Kupoteza fahamu au mtukutiko mwili/kifafa cha mimba
- Kuchoka haraka ,kupumua kwa shida
- Homa
- Mtoto kuacha au kupunguza kucheza tumboni.
- Dalili za ishara za uchungu wa kujifungua
- Mkazo na kuachia kwa misuli ya mfuko wa uzazi unaoendelea kuongezeka na kusababisha maumivu makali ya tumbo na kiuno hadi kujifungua.
- Kutokwa mchozo ute wenye damu.
KUMBUKA: Kama unaishi mbali na kituo cha kutolea huduma za afya ,ni busara kuhamia kwa muda karibu na kituo hicho,kadiri siku ya kujifungua inavyokaribia.
Imeandaliwa na:
DOROTHY A LEMA
MRATIBU WA HUDUMA YA AFYA YA UZAZI NA MTOTO -TANGA