WAUGUZI TANGA RRH WATUNUKIWA VYETI HUDUMA ZA MAGONJWA YA DHARURA NA WAGONJWA MAHUTUTI
Posted on: June 6th, 2025
Picha mbalimbali za matukio wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vyeti kwa wauguzi waliopata mafunzo ya uuguzi kwa wenye dharura yaliyoandaliwa na Shirikisho la Magonjwa ya Dharura nchini (EMAT) ambayo imeendelea kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga kwa pamoja kutoa mafunzo ya huduma za Magonjwa ya dharura na wagonjwa mahututi kwa watumishi wa Hospitali hiyo katika Ukumbi mdogo wa Mikutano uliopo Hospitalini hapa.
Akizungumza Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Dkt. Athuman Kihara amewashukuru EMAT kwa ushirikiano wao ambao wamekuwa wakiutoa kwa wataalam wao katika kuhakikisha wanawajengea uwezo Madaktari na wauguzi hasa inapotokea dharura.
Hafla hiyo fupi ya ugawaji wa vyeti imefanyika mapema siku ya leo Juni 6,2025 huku wauguzi takribani 30 kutoka Idara na Vitengo mbalimbali Hospitalini hapa wakiwa wameshiriki kikamilifu na kutunukiwa vyeti hivyo. Mafunzo hayo ambayo mara kwa mara hufanyika yakihusisha wauguzi na Madaktari kutoka idara tofauti tofauti yana lengo la kuwajengea uwezo hasa pale inapotokea dharura wawapo kwenye maeneo yao ya kazi ikiwa ni jitihada ya Serikali kuhakikisha huduma hizi zinaendelea kuimarika nchini.