Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

WATUMISHI BOMBO WASHIRIKI WARSHA YA WIKI USUGU WA VIMELEA VYA MAGONJWA DHIDI YA DAWA

Posted on: November 19th, 2024

WATUMISHI BOMBO WASHIRIKI WARSHA YA WIKI USUGU WA VIMELEA VYA MAGONJWA DHIDI YA DAWA


Mapema leo Novemba 20,2024 Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Tanga wamefanya Maadhimisho ya Wiki ya Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa Duniani (UVIDA) ambayo huadhimishwa kuanzia tarehe 18-24 Novemba ambapo kwa mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo "Elimisha,Hamasisha,Chukua Hatua Sasa".

Katika warsha ya Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Rodasacks uliopo Hospitalini hapo imefunguliwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt. Frank Shega ambapo awali katika ufunguzi huo amewataka washiriki hao kutumia fursa hiyo kwa Wateja tunaowahudumia kuwashauri matumizi sahihi ya Dawa ili kuepuka madhara yanayotokana na usugu wa dawa.
Amesema "tufanye tafakari kwa sisi wataalam na kutengeneza uelewa kwa jamii juu ya usugu wa Vimelea vya magonjwa dhidi ya Dawa ili kuepuka kusababisha kumuweka mteja katika hali ya matibabu ya muda mrefu na kuliingiza taifa katika gharama ya kutafuta dawa ya kutibu pamoja na kupunguza nguvu kazi ya Taifa".
"Tutimize wajibu wetu kwa kutoa huduma stahiki kwa mgonjwa, kufanya uchunguzi na tafiti ili kumsaidia mgonjwa apone bila ya kumsababishia Usugu wa Vimelea vya magonjwa dhidi ya Dawa ".
Aidha, Prof. Andrew Lusingu kutoka NIMR amesema"Tuielimishe jamii katika kutumia dawa kwa usahihi pamoja na kuacha tabia ya kutumia dawa kiholela bila maelekezo ya Daktari wala kufuata ushauri wa Mfamasia".