Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

WATUMISHI BOMBO WAPATIWA MAFUNZO UHUISHAJI WA MASHINE ZA UCHUJAJI DAMU.

Posted on: April 15th, 2025

WATUMISHI BOMBO WAPATIWA MAFUNZO UHUISHAJI WA MASHINE ZA UCHUJAJI DAMU.

Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo kutoka kada za Uuguzi,Maabara, Madaktari, Lishe na Ustawi wa jamii wamepatiwa mafunzo ya muda mfupi juu ya uhuishaji wa mashine zinazotumika kuchuja damu hospitalini hapo.

Mafunzo hayo yametolewa mapema leo Aprili 16,2025 katika Kitengo hicho na mzabuni Harsh Pharmaceutical Limited yakiongozwa na Mtaalam wa Programu ya Uchujaji damu ( Dialysis Apllication Specialist) Bw. Augustino Mbunda huku yakiwa na lengo la kuboresha huduma kwa wateja wetu wanaofika Hospitalini hapa kwa ajili ya kupata huduma hii.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi hao Mkuu wa kitengo cha Uchujaji damu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bi. Joyce Kapola amesema kuwa "mafunzo haya ni muhimu sana kwetu kwa sababu wawezeshaji hawa wametufundisha namna sahihi ya kuhuisha mashine hizi kwa kila anayehusika kuanzia kwa wafamasia, Maabara, Wauguzi pamoja na Madaktari kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma za tiba kwa wateja wetu wanaofanyiwa dayalisisi au uchujaji damu hospitalini hapa".