Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

WALIOJITOKEZA KAMBI YA INTERPLAST WAANZA KUFANYIWA UPASUAJI.

Posted on: June 14th, 2025



Timu ya Madaktari Bingwa wa Upasuaji kutoka nchini Ujerumani chini ya Shirika lisilo la Kiserikali la Interplast mapema leo Julai 14, 2025 wamekita Kambi ya takribani siku 10 kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kufanya upasuaji wa kurekebisha viungo kwa wenye changamoto mbalimbali hata kufanyiwa upasuaji huo. Timu hiyo yenye jumla ya Madaktari 15 wakiwemo wabobezi Upasuaji rekebishi na plastiki, wauguzi pamoja na madaktari wa usingizi ikiongozwa na Profesa Jurgen Dolderer tayari wameshaanza kufanyia upasuaji wananchi kadhaa waliojitokeza na kujisajili kwa ajili ya huduma hiyo.

Aidha,timu hiyo ya Madaktari kutokea nchini Ujerumani kwa kushirikiana na Wataalam wetu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga wanatarajia kuwafanyia upasuaji wananchi takribani 100 kutokea Mkoa wa Tanga na Mikoa mingine ya jirani wenye changamoto za Mdomo sungura, vidole pacha, makovu sugu, madole bonge, pamoja na uvimbe.

Kambi hiyo ya siku 10 imeanza leo Julai 14, 2025 hadi 25, Julai 2025 huku ikitarajiwa kuwa na neema kwa wananchi wa Mkoa wa Tanga na Mikoa jirani waliojitokeza kupata huduma hizo za upasuaji wa kurekebisha viungo ambapo baadhi ya wananchi wenye changamoto za Uvimbe, na makovu sugu tayari wameshaanza kupatiwa huduma ya upasuaji ili kutatua changamoto hizo zinazozuia utendaji kazi wao.