UONGOZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO WAKABIDHIWA LAPTOP KWA WAKUU WA IDARA
Posted on: February 3rd, 2024Na Mwandishi Wetu, Tanga
UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo katika kuboresha huduma leo umekabidhi vitendea kazi Kompyuta Mpakato (Laptop) kwa Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali kwa ajili ya kuwarahisishia utendaji kazi wao wa kila siku.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo ambapo Matron wa Hospitali hiyo Beatrice Rimoy ambapo aliwakabidhi wakuu wa vitengo mbalimbali vitendea kazi hivyo huko akiwataka kuhakikisha wanavitumia kwenye matumizi yaliyokusudiwa na sio vyenginevyo.
“Leo tunapokea laptop tunakwenda kuzitumia kwenye kazi na sio za kwenda nazo nyumbani kwani zinapaswa kutumika kwenye matumizi yaliyokusudiwa ya kiofisi na sio vyenginevyo Alisema Matron
Alisema hatua ya uongozi wa Hospitali hiyo kukabidhi vifaa hivyo kutokana na kwamba hivi sasa vitu vingi vinaendelea kufanyika kwa kuondoka kwenda kwenye mfumo wa makaratasi na kwenda kwenye mfumo wa mtandao.
“Nitoe wito kwamba mhakikishe mnazitunza lakini kubwa kuhakikisha zinatumika kwenye matumizi yaliyokusudiwa ya Kiserikali na sio vyenginevyo ikiwemo yale ya binafasi”Alisema Matron huyo.
Naye kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Tehama katika Hospitali hiyo William Masika aliwataka kuhakikisha wanatumia kompyuta hizo mpakato kwa ajili ya kuongeza ufanisi na tija katika kuhakikisha taarifa mbalimbali zinajazwa kwa ushahihi.