Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

UWEPO WA MASHINE YA CT -SCAN KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA –BOMBO UMESAIDIA KUPUNGUZA RUFAA ZA WAGONJWA 900

Posted on: February 10th, 2024


SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu imejipambanua kwenye uwekezaji katika maeneo mbalimbali ya kimkakati ikiwemo katika huduma za afya ambapo kuna maboresho makubwa yamefanyika na hivyo kuwezesha huduma kuendelea kuimarika kwenye maeneo.

Si tu katika Hospitali za Taifa  na Kanda lakini pia Hospitali za Rufaa na wilaya ni miongoni mwa ambazo zimenufaika kupitia uwekezaji huo na hivyo kupunguza changamoto ambazo walikuwa wakikutana nazo wananchi awali kufuata baadhi ya huduma nyengine nje ya mikoa yao.

Miongoni mwa uwekezaji huo ni uwepo wa mashine za CT-Scan ambazo ni muhimu kwa kufanya uchunguzi kwa kutumia mionzi ambazo zinatumika kupima vipimo mbalimbali vya kichwa ,ubongo,kifua,tumbo pamoja na mshipa wa damu.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa wanufaika wa uwekezaji huo ambapo kwa kiasi kikubwa umekuwa chachu na hivyo kuondoa changamoto ambazo walikuwa wanakumbana nazo wananchi hususani wa hali ya chini walikuwa wakishindwa kumudu gharama za matibabu.

Athumani Toba ni Mteknolojia wa Mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga  anasema uwekezaji huo uliofanywa na Serikali umesaidia kwa kiasi kikubwa kuwaondolea wananchi adha kubwa waliokuwa wakikutana nayo kulazimika kusafiri nje ya mkoa huo kwa ajili ya kwenda kupata huduma hiyo.

Anasema kwamba uwepo wa CT Scan ambacho ni kifaa muhimu katika kufanya uchunguzi kwa wagonjwa wakiwemo waliopata ajali za barabarani,wagonjwa walipata Shinikizo la damu, vipimo vya kifua ,kuangalia changamoto zilizopo kwenye vifua ikiwemo kufanya uchunguzi na kugundua magonjwa mbalimbali kwenye tumbo uvimbe,kansa na kugundua kansa kwenye utumbo na ubongo.

Toba anasema kitengo hicho kinamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kufanya uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba na hivyo kusaidia kupunguza rufaa  kwa wagonjwa kwenda kupata huduma hizo nje ya mkoa wa Tanga pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt Frank Shega kwa kusimamia huduma hiyo ya CT Scan ambayo imewaondolea wananchi usumbufu wa kuifuata umbali mrefu.

 Akielezea huduma hiyo ilivyoanza anasema ilianza mwezi February mwaka 2023 na mpaka sasa wamekwisha kutoa huduma kwa wagonjwa 900 ambao wangeweza kupewa rufaa kwenye hospitali mbalimbali za nje ya Tanga na hivyo uwepo wake umesaidia kupunguza gharama kwa wateja na usumbufu kwao.

 “Kwa kweli tunaishukuru Serikali kwa hili kwani wagonjwa hao wangelezimika kupatiwa rufaa kwenda nje ya mkoa wa Tanga kupata huduma hizo hivyo tunapenda kuishukuru Serikali kwa uwekezaji huo ambao umesaidia kuondoa kero kwa wananchi wa mkoa wa tanga

Hata hivyo anasema kwa sasa katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Bombo kupitia kitengo cha Mionzi,Idara ya Radiolojia inatoa huduma ya X-ray na Utrasound ambapo huduma za X-ray zinatolewa kuanzia za kawaida na zile maalumu hivyo hivyo kwa Ultrasound   zinatolewa kuanzia zile za kawaida na maalumu na wanafanya ultrasound za wajawazito na magonjwa mbalimbali ya wakina mama na wanaume ikiwemo tezi dume.