Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

TIMU YA UENDESHAJI YA HOSPITALI NA TIMU UDHIBITI UBORA WAPATIWA MAFUNZO YA NYENZO ILIYOBORESHWA YA ISS/5SKAIZEN.

Posted on: June 5th, 2025


Wajumbe wa Menejimenti ya Hospitali (HMT) pamoja na Timu ya Uthibiti Ubora (QIU) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo wamepatiwa mafunzo elekezi kuhusu Internal Supportive Supervision (ISS) na 5S-KAIZEN, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuboresha kasi ya utoaji wa huduma za afya na usimamizi wa ubora wa huduma hospitalini hapa.

Mafunzo hayo yamefanyika mapema leo Juni 05,2025 kwenye Ukumbi mdogo wa Mikutano uliopo hospitalini hapa yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wajumbe hao katika kufanya usimamizi na kuboresha huduma kwa kutumia mbinu shirikishi na katika kutoa Huduma bora kwa wateja wetu.