Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

TANGA RRH KINARA AFYA MAONI FEBRUARI-JUNI:

Posted on: June 4th, 2025



Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo imeibuka kinara ikishika nafasi ya kwanza kati ya 3 katika matumizi ya mfumo wa kukusanya maoni kidigitali unaojulikana kwa jina la Afya Maoni ambao humuwezesha mteja anayetumia mfumo huo kuwasilisha kero, malalamiko au pongezi kulingana na huduma ya afya aliyopata kupitia simu yake ya mkononi.

Katika kikao cha tathmini kilichofanyika mapema leo Juni 4,2025 (jana) katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Hospitalini hapa umeratibiwa na mdau Wezesha pamoja na Serikali kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Tiba kimetoa matokeo hayo mara baada ya tathmini ya muda mrefu tangu kuanzishwa matumizi ya mfumo huo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo.

Katika matokeo hayo kwa kipindi cha Februari hadi Juni jumla ya wateja 450 walijiandikisha katika mfumo wa Afya Maoni huku 122 wakifanikiwa kutoa maoni yao ambapo asilimia 94 ya wateja wetu wakiwa wameridhishwa na huduma.

Aidha tunaendelea kuihamasisha jamii katika matumizi ya mfumo huu wa Afya Maoni katika kutoa maoni juu ya utoaji wa huduma ya afya mara baada ya kufika Hospitalini hapa kwa kutuma ujumbe mfupi tu MAONI kwenda nambari za 15077 kisha fuata maelekezo ya Mhudumu wetu wa Huduma kwa wateja hadi pale utakapokamilisha usajili kisha utapokea dodoso la maswali ndani ya saa nne tu tangu usajili. Huduma hii ni bure na haina makato yoyote kwa watumiaji wa mitandao ya Yas, Airtel na Vodacom.