SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA DUNIANI
Posted on: November 26th, 2024MATUKIO KATIKA PICHA:
Picha za matukio mbalimbali mapema siku ya leo Novemba 28,2024 wakati Timu ya Kupambana na Ukatili wa kijinsia Mkoa wa Tanga wakitoa Elimu ya Ukatili wa Kijinsia kupitia kipindi cha "Amka na TK" kinachoruka kila siku za wiki kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa ikiwa ni muendelezo wa vipindi vya kutoa Elimu kwa Jamii dhidi ya vitendo hivyo katika Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani zilizozinduliwa mapema Novemba 25,2024 huku zikitarajiwa kutamatika Desemba 10,2024.
Elimu mbalimbali zimetolewa na wataalam hao huku ikienda sambamba na kutambulisha Jengo moja la kutolea Huduma Jumuishi kwa manusura wa Ukatili wa Kijinsia lililopo Hospitalini hapa linalokwenda kutatua changamoto na usumbufu wote wanaopitia wahanga wa Ukatili wa kijinsia kwani kituo hicho kitakuwa na kila kitu na kupunguza usumbufu kwa muhanga kupata msaada na utatuzi wa changamoto zake.
Timu hiyo imeongozwa na Bi. Mwanaidi Kombo ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA), Koplo Tabia Matondo na Koplo Happiness Milanzi kutoka Dawati la Jinsia Ofisi ya Kamishna wa Polisi Mkoa wa Tanga na Mmasa Malugu ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Tanga.
Maadhimisho hayo ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia kwa mwaka huu 2024 yana kaulimbiu isemayo " Kuelekea Miaka 30 ya Beijing CHAGUA; Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia".