MATUKIO KATIKA PICHA
Posted on: May 6th, 2025
MATUKIO KATIKA PICHA
Baadhi ya matukio katika picha wakati wa hafla ya kùkabidhi vyeti kwa Watumishi waliohudhuria mafunzo ya Sera na Taratibu za Utumishi wa Umma yaliyotolewa mnamo tarehe 10 hadi 15 Machi 2025.
Vyeti hivyo vimetunukiwa kwa watumishi kutoka vitengo mbalimbali Hospitalini hapa pamoja na watumishi wapya katika kada za Uuguzi, Maabara pamoja na Madaktari baada ya kuhudhuria mafunzo hayo kikamilifu yenye lengo la kuwaongezea maarifa pamoja na maadili ya utumishi wa umma katika kuwahudumia wananchi.
Akizungumza katika hafla hiyo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt. Frank Shega amewataka watumishi hao kuendelea kukumbuka yote waliyofundishwa na wakufunzi hao pamoja na kuyasimamia ili kuepuka kufanya makosa ya kimaadili ya utumishi wa umma na badala yake tufanye kazi kwa bidii na kuwahudumia wateja wetu wanaofika Hospitalini hapa kupata huduma mbalimbali na tukiwaacha wakiwa wameridhika na huduma zetu.