Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

MADAKTARI BINGWA BOMBO WAFANYA UPASUAJI KUWEKA NYONGA BANDIA

Posted on: May 2nd, 2024


MADAKTARI BINGWA BOMBO WAFANYA UPASUAJI WA KUWEKA NYONGA BANDIA.

Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Mifupa wa Dkt Samia Kanda ya Kaskazini wakiwa kwenye chumba Cha Upasuaji ili kuweka nyonga bandia.

Upasuaji huu umefanyika leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ikiwa ni muendelezo wa kutoa huduma za Matibabu ya kibingwa na Ubingwa bobezi kwa wananchi wa Mkoa wa Tanga na Mikoa ya jirani kwenye Kambi maalum ya Matibabu ya Madaktari Bingwa wa Dkt Samia Kanda ya Kaskazini waliopo hapa Hospitalini kuanzia ile siku ya Jumatatu ya Aprili 29,2024.

Dkt Tumaini Minja kutoka Taasisi ya Mifupa (MOI) ameongoza zoezi hilo la Upasuaji akishirikiana na Dkt Tumaini Minja kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo) ambae ni Daktari Bingwa katika Viungo vya Mifupa pamoja na wasaidizi wengine.

Kambi hii ya Matibabu ya Kibingwa ilianza kutolewa hapa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga tangu tarehe 29/04/2024 na inahitimishwa Ijumaa ya tarehe 03/5/2024.

Huduma za Magonjwa zinazotolewa ni pamoja na Magonjwa ya Upasuaji, Mifupa, Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Magonjwa ya Saratani, Magonjwa ya Watoto, Magonjwa ya Masikio,Pua na Koo, Magonjwa ya Macho, Magonjwa ya Kinywa na Meno, Magonjwa ya Ngozi, Magonjwa ya Mfumo wa Mkojo, Magonjwa ya ndani (sukari,shinikizo la juu la damu na mengineyo) pamoja na Magonjwa ya Afya ya akili.