Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA YATEMBELEA CTC-BOMBO

Posted on: April 14th, 2025

KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA YATEMBELEA CTC-BOMBO

Kamati ya Kudhibiti UKIMWI Halmashauri ya Jiji la Tanga ikiongozwa na Madiwani na wataalam mbalimbali mapema leo Aprili 15,2025 wametembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga katika kitengo cha Huduma tiba na Matunzo (Care and Treatment Clinic-CTC) kwa ziara ya kupokea taarifa juu ya utoaji wa huduma za tiba na matunzo kwa WAVIU pamoja na ushirikishwaji wa viongozi na jamii katika kupambana na kudhibiti kasi ya maambukizi ya VVU.

Akisoma taarifa hiyo ya Hospitali Dkt. Elisei Magiri ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma tiba na Matunzo kwa WAVIU amesema "Hadi kufikia mwezi huu April 2025,Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga katika kitengo cha CTC kina jumla ya wapokea huduma ambao ni WAVIU 3432 ambao ME ni 1105 na KE ni 2327 na kati yao kuna jumla ya watoto 204 kati yao ME ni 104 na KE 100".

"Katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2025 tumeweza kuanzisha dawa Kinga za TB kwa wapokea huduma wapya Jumla 22 na kuwaanzishia matibabu wapokea huduma WAVIU waliogundulika kuwa na Ugonjwa wa TB watano. Kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2024 tumeanzisha dawa Kinga za TB kwa wapokea huduma WAVIU wapya Jumla 34 na kuanzishia matibabu kwa wapokea huduma WAVIU waliogundulika na TB watano( 5)".

"Aidha akizungumzia mafanikio katika kitengo hicho Dkt. Magiri amesema "tumefanikiwa kuwaanzishia kwa wakati sahihi huduma za tiba na matunzo kwa wale wote waliogundulika na maambukizi,Huduma za msamaha kwa WAVIU zimetolewa pale zinapohitajika kwa kupitia dirisha la ustawi wa jamii, kuwasimamia wateja wetu katika unywaji mzuri wa dawa na kupelekea kufubaza virusi kwa 97.38%,Muda wa kusubiria majibu ya HVL umepungua baada ya hospitali kuanza kupima hapa kwenye Maabara yetu pia Serikali imeunganisha huduma za Homa ya Ini(Hepatitis virus Cares) na HIV,hivyo imesaidia kuwapa dawa kwa bila malipo kwani awali walikuwa wananunua ".

Pia, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Bombo Dkt. Abdi Msangi amewashukuru kamati hiyo kwa kuja kutembelea katika Kitengo hicho na kupata taarifa za hali ya utoaji huduma kitengoni hapo kwa maslahi mapana ya wananchi wetu wanaopata huduma hizi.