HOSPITALI YAKABIDHIWA VITI TOKA TPPL
Posted on: December 19th, 2019Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, imekabidhiwa Viti vya kukalia wateja wakati wakisubiri huduma. Viti hivyo vimetolewa na Kampuni ya Tanga Pharmacetical and Plastic Limited (TPPL) na kukabidhiwa na Afisa Rasilimali watu wa kampuni hiyo Bi. Jenipher A. Mburuja. Wakati wa kukabidhi viti hivyo, Bi Jenipher Mburuja alisema kama kampuni wanajisikia furaha katika kupata nafasi ya kushiriki katika kuboresha Huduma zinazotolewa hospitalini hapo. Aidha Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Dr. Naima Zakaria ameshukuru kwa msaada huo na kuhakikisha kuwa viti hivo vitatumika kwa makusudi yaliyokusudiwa ili kuboresha huduma katika hospitali yetu.