Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

HOSPITALI YA BOMBO YAKABIDHIWA KISIMA KINGINE CHA MAJI.

Posted on: March 10th, 2025

HOSPITALI YA BOMBO YAKABIDHIWA KISIMA KINGINE CHA MAJI.

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo mapema leo Machi 11,2025 imekabidhiwa kisima kingine cha maji kutoka kwa mdau Master One Family kwa kushirikiana na msimamizi wa mradi huo Ndg. Rahim Ibrahim kwa ajili ya kusaidia kupunguza adha ya maji kwa shughuli za Hospiali hapo. Kisima hicho ni cha pili kukabidhiwa kwa Hospitali ya Bombo baada ya kile cha kwanza kilichozinduliwa na kukabidhiwa na Mhe. Japhari Kubecha Mkuu wa wilaya ya Tanga mnamo tarehe 19, Februari 2025.

Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt. Athumani Kihara amemshukuru mdau Taasisi ya Master One Family kwa kuwachimbia kisima hicho cha maji hadi utengenezaji wa miundombinu huku kisima hicho kikitarajiwa kupunguza wingi wa malipo katika kulipa ankara za maji.

"Naomba nitumie fursa hii kuwashukuru wadau taasisi ya Master One Family kwa kwa ajili ya ujenzi hadi kukamilika kwa miundombinu ya maji kwenye kisima hicho kwani kupitia kisima hiki tunakwenda kupunguza gharama za ulipaji wa ankara za maji, hivyo naomba pia wadau wengine kuguswa kuchimba visima vingine ili kurahisisha hali ya upatikanaji wa maji Hospitalini hapa.

Pia, kwa upande wake mwakilishi wa Mdau Taasisi ya Master One Family Ndg. Rahim Ibrahim amesema kuwa kisima hicho ni utekelezaji wa yale waliyoahidi katika kuboresha Huduma za maji Hospitalini hapo huku akiwakumbusha kukifanyia maboresho na ukarabati kila baada ya miezi sita kuanzia sasa ili kuendelea kupata huduma za maji zaidi na zaidi.