HOSPITALI YA BOMBO KUJA NA MFUMO MPYA WA UKUSANYAJI WA MAONI KIDIGITALI.
Posted on: March 4th, 2025
HOSPITALI YA BOMBO KUJA NA MFUMO MPYA WA UKUSANYAJI WA MAONI KIDIGITALI.
Matukio mbalimbali mapema leo Machi 05,2025 katika usambazaji na utoaji wa elimu kuhusiana na mfumo mpya wa ukusanyaji wa maoni unaojulikana kwa jina la "Afya Maoni" utakaotumika kwa wateja wanaofika Hospitalini hapa kutoa maoni yao kwa kuandika ujumbe mfupi tu MAONI kisha fuata maelekezo mengine.
Sambamba na elimu hiyo Timu ya wataalam kutoka kada mbalimbali Hospitalini hapa wameshirikiana katika kuelekeza kwa vitendo na kugawa vipeperushi maalum vyenye maelekezo ya jinsi ya kutumia mfumo huu wa Afya Maoni utakaowasaidia kutoa maoni,kero au pongezi kupitia ujumbe mfupi ambao ni bure pasipo kutozwa gharama yoyote ile.
Katika kuboresha kasi na ufanisi wa utoaji huduma za Afya kwa wateja sasa unaweza kutuma Ujumbe mfupi kupitia nambari 15077 tuma neno MAONI kisha fuata maelekezo ya Mhudumu wetu wa Huduma kwa wateja hadi mwisho.
Ni Rahisi Sana!!.