Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

Hospitali ya Bombo Kuanza kutoa huduma ya kusafisha Figo

Posted on: November 16th, 2019

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipatia Hospitali ya Bombo Mashine Tano zitakazo tumika kwa ajili ya kutolea huduma ya usafishaji Figo. Mashine hizo zitasaidia kupunguza usumbufu na gharama kwa wagonjwa wenye uhitaji wa huduma hiyo kwa kuwa kwa sasa inawalazimu kuifuata katika hospitali za Kanda au Hospitali ya Taifa Muhimbili. Katika Kujiandaa na utoaji wa huduma hiyo, Uongozi wa Hospitali umepeleka watumishi watano katika mafunzo juu ya utoaji wa huduma hiyo na kuanza kuweka mazingira mazuri yatakayotumika kutoa huduma hiyo. Huduma hiyo inatarajiwa kuanza kupatikana mwezi disemba 2019.