HONGERA WAFANYAKAZI HODARI
Posted on: May 15th, 2025
HONGERA WAFANYAKAZI HODARI
Baadhi ya matukio katika picha wakati wa hafla ya kùkabidhi vyeti kwa Watumishi na Idara mbalimbali walioibuka vinara katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu wanaofika Hospitalini hapa kupata huduma zetu.
Vyeti hivyo vimetunukiwa mapema leo Mei 16,2025 katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Bombo kwa watumishi binafsi kutoka kwenye Idara na vitengo mbalimbali Hospitalini hapa huku Idara za Maabara,Watoto na Radiolojia zikiibuka vinara katika kutoa huduma bora kwa wateja.
Akizungumza katika hafla hiyo wakati wa kukabidhi vyeti Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt. Frank Shega amewaasa watumishi katika Hospitali ya Bombo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwahudumia wananchi wetu kwa kufuata Sheria,kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma.