Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

DKT SHEGA: WAUGUZI FUATENI MAADILI NA MIIKO YA KAZI.

Posted on: June 12th, 2025



Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt. Frank Shega amewataka wauguzi kufuata maadili na miiko ya kazi wakati wa kuwahudumia wagonjwa. Ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani ambapo tawi la Bombo limeadhimisha leo Juni 12,2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Afya Bombo.

"Niwasihi wauguzi kufuata maadili na miiko ya fani ya uuguzi pale tunapowahudumia wateja wetu pamoja na kufanya kazi kwa bidii kuanzia chini na kuchukua hatua stahiki kuwahudumia wateja wetu ili kufikia lengo letu la kutoa huduma bora".

Amesema "Kushirikiana na watu wa kada nyingine ili kupunguza matabaka na tuwe kitu kimoja na tumaanishe tunaposema wauguzi ni nguvu ya mabadiliko na nawaahidi kuyafanyia kazi yote mliyoyawasilisha kwangu bila upendeleo pamoja na kuboresha mazingira yetu ya kufanyia kazi ili kuwapunguzia msongo wa mawazo mahali pa kazi".

Aidha, maadhimisho hayo yameenda sambamba na mazoezi mbalimbali ikiwemo kuwasha mishumaa na kula kiapo kwa watumishi wa fani uuguzi pamoja na kutoa zawadi kwa wagonjwa mbalimbali katika wodi za upasuaji kwa wanaume.