Nafikaje Hospitali ya Bombo?
Hospitali ipo pembezoni mwa Bahari ya Hindi, Karibu na Bandari ya Tanga eneo la Bombo kwenye barabara ya Hospitali. Ukitokea Mjini unaweza panda daladala za kwenda Raskazoni na utashukia kituo cha Bombo Hospitali, Hapo utaona Geti la kuingia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga.