Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

WATAALAM MAABARA BOMBO WAMALIZA RIPOTI YA UCHUNGUZI WA MAZINGIRA

Posted on: May 14th, 2026

Katika hatua muhimu inayolenga kuimarisha usalama na ubora wa huduma za afya, wataalam wa Maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo leo Mei 14,2026 wamekamilisha uwasilishaji wa ripoti ya kina kuhusu uchunguzi wa mazingira katika maeneo yanayoguswa sana ya maji na hewa ndani ya Hospitali.

Ripoti hiyo, ambayo ilianza kuwasilishwa wiki iliyopita, imetoa maelezo ya kina na mapendekezo yanayolenga kuhakikisha mazingira ya Hospitali yanabaki salama kwa wagonjwa, watumishi na wageni wote.

Uchunguzi umelenga hasa maeneo yanayohusiana na ubora wa maji na hewa, ambayo ni muhimu sana katika kudhibiti maambukizi na kutoa mazingira bora kwa mteja.

Aidha,Menejimenti ya  Hospitali ya Bombo imewataka watumishi wote kuzingatia kwa dhati utoaji wa huduma bora na za kiwango cha juu kwa wananchi ili kuhakikisha Hospitali inabaki kuwa mahali pa matumaini na uponyaji.

Hatua hii inaonesha dhamira ya dhati ya uongozi wa Hospitali katika kutoa huduma za afya zinazozingatia viwango vya kimataifa na mahitaji ya wakazi wa Mkoa wa Tanga.