Ukaribisho
Dr. Frank Damas Shega (MoIC)
Karibu Tanga RRH
Karibu sana Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Hospitali hii ipo mwambao wa Bahari ya Hindi, Ina mandhari mazuri na ya kihistoria. Mategemeo yetu ni kukupatia huduma unayostahili bila kujali tabaka lolote la Dini, Kabila, Kipato, Rangi, Jinsia, Umri wa Taifa unalotoka. Mteja wetu tutamuhudumia kwa kufuata weredi wa kutoa huduma, miongozo na taratibu za nchi kwa kusimamia usawa na haki. Ni vema pia kama hukuridhika na huduma zetu, tupe mrejesho kwa kufuata utaratibu wa Hospitali wa kukusanya taarifa kutoka kwa wateja ili tuweze kujirekebisha na kuboresha huduma zetu. Ahsante sana. Karibu Tukuhudumie.
Dr. Frank Damas Shega
Mganga Mfawidhi wa Hospitali