Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

WATUMISHI BORA WATUNUKIWA TUZO HOSPITALI YA BOMBO.

Posted on: July 29th, 2026

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo, Dkt. Frank Shega, leo Julai 30, 2026, amewatunuku tuzo na zawadi mbalimbali watumishi waliofanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao.

Watumishi hao walitambuliwa kutokana na utendaji wao bora katika vipindi vya tathmini vya Aprili-Juni 2025 na Julai-Septemba 2025.


Akizungumza baada ya kukabidhi tuzo hizo, Dkt. Shega amewapongeza watumishi hao kwa kujituma na kuwataka waendelee kudumisha bidii, weledi na uwajibikaji katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Aidha, ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wakuu wa idara kuhakikisha watumishi wanafanya kazi kwa kuzingatia matumizi sahihi ya kumbukumbu na nyaraka za kazi, hatua itakayochangia kuongeza ufanisi, uwajibikaji na ubora wa huduma zinazotolewa hospitalini.


Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga - Bombo, imekuwa na utaratibu wa kutoa Tuzo kwa watumishi wake ili kutambua na kuhamasisha utendaji bora, kujitolea, na kujituma katika kuboresha afya za jamii.


Hongera kwa watumishi wote waliotambuliwa na endeleeni kuwa chachu ya utendaji bora na utoaji wa huduma zenye viwango vya juu.