Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

TATHMINI YA MATIBABU-CLINICAL AUDIT KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA-BOMBO

Posted on: August 5th, 2026

Picha mbalimbali ambapo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo imekamilisha zoezi la tathmini ya matibabu-Clinical Audit lililoendeshwa na Wizara ya Afya kwa siku mbili na kuhitimishwa leo, Agosti 5, 2026.

Tathmini hiyo imeonesha maboresho makubwa katika utoaji wa huduma za afya na usimamizi wa nyaraka za wagonjwa, ikiakisi jitihada za hospitali za kuendelea kuimarisha ubora wa huduma.

Akizungumza baada ya kupokea matokeo ya tathmini hiyo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali, Dkt. Frank Shega, amesema zoezi hilo ni fursa muhimu ya kujitathmini, kubaini maeneo ya kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Pia amewahimiza watumishi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi, kuzingatia miongozo ya kitaalam na kuhakikisha nyaraka za wagonjwa zinajazwa kwa usahihi kila wanapotekeleza majukumu yao.