Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

NAMNA BOMBO ILIVYOGUNDUA KESI YA MINYOO KUSABABISHA DEGEDEGE.

Posted on: September 8th, 2026

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo imefanikiwa kubaini na kutibu kesi adimu ya kijana mwenye umri wa miaka 25 aliyekuwa akipata degedege na kupoteza fahamu, hali iliyohusishwa na maambukizi ya minyoo aina ya Ascaris lumbricoides.

Kwa mujibu wa utafiti ulioandikwa na Dkt. Shabbir Moizali wa Hospitali ya Bombo, mgonjwa huyo alifika hospitalini akiwa na degedege za mara kwa mara na kupoteza fahamu, huku vipimo mbalimbali  vikishindwa kubaini chanzo cha hali hiyo.

Mgonjwa alianza matibabu kwa kutumia dawa ya albendazole na Siku ya tatu alitoa minyoo kadhaa kupitia kinyesi, ambayo ilitambuliwa kuwa Ascaris lumbricoides. 

Baada ya hapo, hakupata tena degedege wala kupoteza fahamu na alipata nafuu kabisa.

Utafiti huo ulichapishwa katika Jarida la International Journal of Research and Scientific Innovation-IJRSI mwaka 2024, ukiweka kumbukumbu ya kesi hii adimu iliyoshughulikiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo.

SOMA ZAIDI KUPITIA KIUNGANISHI HIKI ILI KUONGEZA  ELIMU NA MAARIFA KUHUSU AFYA.

https://rsisinternational.org/journals/ijrsi/articles/an-unusual-case-of-ascariasis-induced-convulsions-and-unconsciousness-in-a-young-adult-male-at-tanga-regional-referral-hospital-in-tanzania/