BOMBO YAFANIKIWA KUTOA UVIMBE WA KILO 3.5 KWA MWANAMKE MWENYE MIAKA 38.
Posted on: August 17th, 2026Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo imefanikiwa kufanya upasuaji na kuondoa uvimbe wenye uzito wa kilo tatu na nusu uliokuwa ndani ya kizazi cha mwanamke mwenye umri wa miaka 38, aliyekuwa akisumbuliwa na hali hiyo kwa muda mrefu.
Akizungumza kuhusu upasuaji huo uliodumu kwa takribani saa moja, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dkt. Mazina Mwajabu, amesema uvimbe huo ulikuwa mkubwa na ulipatikana ndani ya kizazi.
Dkt. Mazina amesema mwanamke huyo hajawahi kupata mtoto katika maisha yake, huku akieleza kuwa uvimbe wa aina hiyo unaweza kuwa miongoni mwa sababu zinazoweza kuathiri uwezo wa mwanamke kupata ujauzito.
Upasuaji huo umefanikishwa na wataalam wanne kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo, ambao walishirikiana katika hatua mbalimbali za matibabu.
Kwa sasa, mgonjwa anaendelea kufuatiliwa na wataalam wa hospitali, huku hali yake ikiendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji huo.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo hutoa huduma za kliniki kwa watu wenye changamoto za ugumba na utasa kila siku ya Alhamisi, ambapo wagonjwa hupatiwa uchunguzi, ushauri na matibabu kulingana na hali zao



