Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

BOMBO YAANDIKA HISTORIA KWA KUFANYA KIPIMO CHA BRONCHOSCOPY KWA MARA YA KWANZA

Posted on: August 7th, 2026

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo imeandika historia kwa kufanya kwa mara ya kwanza kipimo cha Bronchoscopy, huduma ya kibingwa inayotumia mashine ya Endoscopy kuchunguza njia ya hewa kwa kutumia kamera maalum.

Kipimo hicho hufanyika kwa kuingiza kamera ndogo kupitia njia ya hewa ya mgonjwa ili kuchunguza kwa usahihi kubaini chanzo cha tatizo na kuwezesha madaktari kutoa matibabu sahihi kwa wakati.

Akizungumza baada ya kufanikisha zoezi hilo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo, Dkt. Mohamed Sachedine, amesema hospitali imefanikiwa kumfanyia mgonjwa wa kwanza kipimo hicho.

Huduma hiyo ni sehemu ya jitihada za Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo za kuendelea kuimarisha huduma za uchunguzi na matibabu kwa kutumia teknolojia za kisasa, ili kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi.