Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

BOMBO NA ROTARY CLUB WAENDESHA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU SALAMA.

Posted on: July 28th, 2026

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo, kwa kushirikiana na Rotary Club ya Tanga Mjini, Julai 26, 2026 iliendesha zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lililofanyika katika Ukumbi wa Hindu Mandal, jijini Tanga.

Wakati zoezi hilo likiendelea, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Buriani@@batilda.burian ,alitembelea eneo la tukio na kuwapongeza waandaaji kwa juhudi za kuhamasisha jamii kushiriki katika uchangiaji damu salama.

Balozi Dkt. Buriani aliipongeza Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo kwa kuendelea kuwa kinara katika uratibu na uhamasishaji wa shughuli za uchangiaji damu salama mkoani Tanga na kwamba juhudi hizo zina mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya wananchi wanaohitaji huduma hiyo.

Zoezi hilo limeendelea kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya afya na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha upatikanaji wa damu salama kwa wakati, hatua inayochangia kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya wananchi.