Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

HUDUMA ZA LISHE

Posted on: April 19th, 2024

Kutoa elimu kwa wagonjwa na wateja wanaohudhuria hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga.

  • Elimu ya unyonyeshaji .
  • Kumnyonyesha mtoto ndani ya saa moja baada ya kujifungua na faida zake.
  • Kunyonyesha mtoto mfulululizo miezi 6  bila kumpa kitu chochote faida zake, jinsi ya kufanikisha zoezi hili kwa vitendo .
  • Umuhimu wa mtoto kupelekwa kliniki na kupatiwa chanjo.
  • Elimu ya uanzashaji wa vyakula vya nyongeza,namna ya kuviandaa na namna ya kumlisha mtoto, kwa watoto kuanzia umri wa miezi 7 na kuendelea.
  • Elimu ya ulaji ulio sahihi kwa wateja kulingana na tatizo la mteja na kuwapima uzito na urefu kwa ajili ya kuangalia uwiano (BMI) hasa kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na uzito uliozidi na kufanya ufuatiliaji.
  • Kisukari
  • Moyo
  • Shinikizo la damu
  • Saratani
  • Elimu namna bora na umuhimu wa ufanyaji wa mazoezi.
  • Tunatoa elimu lishe kwa wazee waohudhulia kliniki za magonjwa mbalimbali au wanaokuja kutibiwa namna nzuri ya kukabiliana na changamoto za uzee na lishe bora kwa wazee.
  • Tunatoa elimu lishe kwa wagonjwa mbalimbali waliolazwa hospitalini kulingana na mahitaji yao

Tunatoa huduma ya matibabu ya utapiamlo wa kadiri na mkali.

  • Tunawalaza watoto wenye utapiamlo mkali na kuwapa matibabu yafuaatayo
  • Tunawatengenezea maziwa maalumu kwa ajili yao yanaitwa F75 maziwa ya kuanzia na F100 maziwa yanayofuatia na baada ya hapo kuhamia kwenye chakula dawa.
  • Tunawapima uzito kila siku ili kuangalia mabadiliko yanayotokea kwa mtoto na kutoa tiba iliyo sahihi
  • Kwa wale wenye utapiamlo mkali ikiambatana na kuharisha tunawetengenezea dawa yenye mchanganyiko wa Resomal na maji kusaidia kurudisha kiwango cha maji na  madini kilichpotea mwilini.
  • Tunawashauri akina mama au walezi waliolazwa na mtoto kuhakikisha anapata joto kila wakati kwa kuwafunika nguo za kutosha.
  • Kwa wale ambao wanakuja wamefikia mpaka hatua ya kuwa vidonda mwilini tuna waogesha kwa kutumia potassium per manganate.
  • Tunawasaidia watoto kwa kuwapa vitu vya kuchezea mfano mwanasesere ,magari,mpira ili kujiridhisha kama mtoto ameshapona tayari kwa kuruhusiwa kwenye nyumbani na kuhudhuria kituo cha karibu kwa kuendelea kufuatiliwa

Tunatoa huduma ya uchunguzi na ushauri baada ya kujifungua kwa kushirikiana na mratibu wa mama na mtoto.

  • Tunamchunguza mama kama ana upungufu wa damu , kama anao anarudishwa kwa daktari kwa uchunguzi na kama hana basi anapewa ushauri wa ulaji uliosahihi ili aweze kuongeza damu yake zaidi.
  • Anapewa elimu ya unyonyeshaji na namna bora ya unyonyeshaji, na vyakula gani ale ili kusaidia kuzalisha maziwa kwa wingi.
  • Tunamshauri pia namna ya kufanikisha zoezi la unyonyeshaji .
  • Anapewa matone ya vitamin A
  • Tunatoa huduma ya chakula kwa wagonjwa wanaotoka mbali na hapa Tanga jiji na kama mgonjwa hana ndugu wa karibu wa kumhudumia .Chakula hiki kinatolewa kulingana na mahitaji ya mgonjwa.
  •  
  • Tunasimamia na kuhakisha chakula hiki ni bora na ni salama kwa mgonjwa.
  • Tunawajengea uwezo wapishi wetu namna ya kupika vyakula mbalimbali vya waonjwa na uaandaaji wake.
  • Tunahakikisha wapishi wamipwa afya zao kwa usalama wa chakula kwa mgonjwa