Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

HUDUMA YA MAGONJWA YA AKILI NA USHAURI

Posted on: March 29th, 2024

Jengo la Kitengo cha Magonjwa ya Akili

HUDUMA ZINAZOTOLEWA KATIKA KITENGO CHA AFYA YA AKILI

  • Huduma za wagonjwa wa nje
  • Huduma kwa wagojwa waliolazwa wodini
  • Huduma kwa wagonjwa wa akili majumbani
  • Tiba shufaa kwa wagojwa wa akili (occupational therapy)
  • Huduma ya tiba za kisaikolojia (psychotherapy)
  • Utoaji wa Elimu kwa jamii kuhusu magonjwa ya akili na dawa za kulevya

HUDUMA ZA WAGONJWA WA MAJUMBANI

Huduma za wagonjwa wa akili majumbani hutolewa kwa kuwatembelea wagonjwa wa akili majumbani. Huduma hii imeanza kutolewa toka mwaka 2011 kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali HAMA chini ya TICC.

Lengo likiwa kutoa elimu kwa familia na jamii kuhusu magojwa ya akili.

Kufuatilia ufuasi wa dawa kwa mgojwa na familia kujua umuhimu wa dawa kwa mgonjwa

Kupunguza unyanyapaa kwa wagonjwa wa akili.`

KUTOA ELIMU YA AFYA YA AKILI NA DAWA ZA KULEVYA KWA JAMII

  • Elimu hutolewa kwa jamii kwa njia mbalimbali kama zifuatazo
  • Kutumia vyombo vya habari
  • Kuongea na  watumiaji wa dawa za kulevya kwenye vijiwe vyao
  • Mashuleni kuongea navijana kuhusu daawa za kulvya na magonjwa ya akilia
  • Kufikisha ujumbe kwa njia ya michezo ya kuigiza