Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

MAMIA WAJITOKEZA HOSPITALI YA MAWENZI KAMBI YA MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA KANDA YA KASKAZINI

Posted on: December 2nd, 2024

MAMIA WAJITOKEZA HOSPITALI YA MAWENZI KAMBI YA MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA KANDA YA KASKAZINI

Wananchi takribani 1300 wamejitokeza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mawenzi kukutana na Madaktari Bingwa wa Dkt.Samia kutoka Kanda ya Kaskazini walioweka Kambi  Hospitalini hapo kwa muda wa siku tano kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro na jirani.

Kambi hiyo imezinduliwa rasmi siku ya leo Desemba 04, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Nurdin Babu imekuwa kivutio kwa wananchi wengi kufika hospitalini hapo kupata huduma za kiuchunguzi na za kibingwa kutoka kwa wataalam 60 wanaohudumu katika kada mbalimbali.

"Wanachi wa Mkoa wa Kilimanjaro tuitumie fursa ya Kambi hii ya madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi kupata huduma Bora na za kitaalam".

Amesema hayo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu wakati Akifungua Kambi ya siku 5 ya madakari bingwa na Bobezi wa Mhe. Rais Samila Suluhu Hassan katika Viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi.

Aidha, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi Dkt Edina-Joy Munisi amesema tayari wagonjwa 1328 wamepata huduma hii ya Madaktari Bingwa huku wengine 22 wamefanikiwa kufanyiwa upasuaji.

Kambi hiyo ya Madaktari Bingwa na Mabingwa bobezi Kanda ya Kaskazini inayojumuisha Hospitali za Rufaa za Tanga,Mawenzi,Mount Meru,Manyara,Kibong'oto na Hospitali ya Taifa Muhimbili ni moja ya Kambi nyingi zinazoendelea nchi nzima katika kuimarisha hali ya uboreshaji wa huduma za Afya kwa wananchi wake.