Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

AONDOLEWA UVIMBE WA KILOGRAMU 5 KAMBI YA MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA KANDA YA KASKAZINI.

Posted on: December 6th, 2024

AONDOLEWA UVIMBE WA KILOGRAMU 5 KAMBI YA MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA KANDA YA KASKAZINI.

Mnufaika mmoja wa Kambi ya Matibabu ya Madaktari Bingwa na Mabingwa bobezi Kanda ya Kaskazini aliyejulikana kwa majina ya Jackline Mikeli (32) ambaye ni raia wa nchini Kenya katika Mji wa Mombassa amefanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe wenye takribani kilogramu 5 uliokuwa ukimsumbua kwa takribani miezi kadhaa sasa.

Amesema aligundua ana tatizo hilo alipokuwa nchini Oman, na aliporudi nyumbani (Kenya) alisikia kuwepo kwa Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi Kanda ya Kaskazini na kuamua kuja kupata huduma za kibingwa kutoka kwa Madaktari hao walioweka Kambi ya siku tano katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mawenzi.

Akiongea mara baada ya upasuaji huo Daktari Bingwa wa magonjwa ya Wanawake na Uzazi Dkt. Victor Adolph amesema "Uvimbe huo umemsumbua toka mwezi wa tisa mwaka huu 2024 hadi siku ya jana tulipofanikiwa kumfanyia upasuaji wa kuondoa uvimbe huo".

Aidha, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi Dkt Edna-Joy Munisi ameishukuru Serikali kwa kufanikisha kuweka na kuratibu kambi ya Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi kwani zimefikisha huduma za afya za kibingwa kwa wananchi na wamenufaika kwa huduma hizo.